Kartra

Yanga Wafungukia Ishu ya Mukoko na Horoya

BAADA ya kuzuka tetesi nyingi kwenye mitandao ya kijamii juu ya tetesi kumuhusu kiungo wao mkabaji Mukoko Tonombe kuhitajika na Klabu ya Horoya ya Guinea uongozi wa Yanga umesema haujapokea ofa yoyote na wao wanaona tu mitandaoni.

 

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema hawajui chochote kuhusu suala hilo na wenyewe wanaona kwenye mitandao ya kijamii na kwamba hawajapokea taarifa yoyote juu ya Horoya kumtaka mchezaji wao.

 

Bumbuli alisema kama Horoya wanamtaka Mukoko watawatafuta na kukaa nao chini kuzungumza nao lakini kwa sasa wameelekeza nguvu kwenye michezo ya Azam Sports Federation Cup na michezo ya ligi kuu.

 

“Hakuna hiyo taarifa kwetu kuwa Horoya wanamtaka Mukoko. Ni taarifa ambazo hata sisi tunaona kwenye mitandao ya kijamii lakini hakuna ofa yoyote, macho yetu kwa sasa tunawaza michezo yote ambayo ipo mbele yetu,” alisema.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam


Toa comment