Yanga, Wahispania Mambo Mazuri Yamefikia Hapa

KAMPUNI ya La Liga ya nchini Hispania wanatarajiwa kukabidhi ripoti ya mwisho ya mapendekezo yao kwa uongozi wa Yanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti Mkuu wa timu hiyo, Dr Mshindo Msolla.

 

La liga ndiyo wamepewa jukumu la kupendekeza mfumo wa uendeshaji wa klabu ya hiyo baada ya hivi kuingilia makubaliano mazuri ya kushirikiana katika masuala ya kimichezo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa Oktoba, mwaka huu mapema wataipokea ripoti hiyo kutoka La liga kupitia klabu ya Sevilla ya nchini Hispania.

 

Mwakalebela alisema kuwa mchakato umefikia hatua nzuri na ripoti hiyo ni ya mwisho tayari kuelekea hatua inayofuata katika kukamilisha mchakato huo wa mfumo wa mabadiliko.

 

Aliongeza kuwa baada ya hatua ya kwanza ya makabidhiano, watapata utaalamu wa ndani, na baadaye watautoa nje kwa kushirikisha matawi yote ya Yanga nchini nzima.

 

“Baada ya kupata utaalamu huo katika matawi yote ya Yanga kuelimisha na kupata ushauri wa wanachama kutokana na ripoti hiyo baadaye itapelekwa katika mkutano mkuu kupata ridhaa ya wanachama wote.

 

“Niwatake wanachama wa Yanga, kuunga mkono mabadiliko hayo ya kimfumo kwa sababu baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo tutawashirikisha wanachama wetu kabla ya kupeleka katika mkutano mkuu.

 

“Kikubwa wanachama wajitokeze kwa wingi kusapoti timu yao ikiwa ni pamoja na kununua jezi halali na kujitokeza kwa wingi katika viwanja inapocheza timu yao,” alisema Mwakalebela.

Stori: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

KUMEKUCHA! MASHABIKI wa SIMBA, YANGA Watema CHECHE, WALAANI Vitendo vya VURUGU za MASHABIKI wa YANGA

Toa comment