Yanga Walamba Kitita cha Milioni 405 kutoka kwa Mdhamini wao Mkuu, SportPesa
Rasmi Young Africans SC imepokea Hundi ya TZS 405,000,000/= (milioni mia nne na tano) kutoka kwa mdhamini mkuu wa Klabu @tzsportpesa kama sehemu ya fedha za mafanikio ya Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam na Mashindano ya CAF.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya pesa hizo, Mkurugenzi wa bodi ya Wawekezaji kutoka SportPesa, Abbas Tarimba(Mb) amesema kwamba wanakabidhi zawadi ikiwa ni sehemu ya shukrani zao kwa klabu ya Yanga kwa mafanikio waliyoyapata katika mashindano mbalimbali ya ndani na yale ya kimataifa kwa msimu uliopita.

