The House of Favourite Newspapers

Yanga Wazindua Jezi Mpya Msimu 2020/21 (Picha+Video)

0

YANGA kwa kushirikiana na kampuni ya GSM, leo Septemba 11, 2020,  wametambulisha jezi  watakazozitumia msimu wa 2020/21.

 

Hafla hiyo imefanyika leo asubuhi makao makuu ya timu hiyo Jangwani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela,  alisema kuwa hizo ndizo jezi rasmi na halali za Yanga watakazozitumia  msimu ujao.
Amesema jezi hizo zina ubora mkubwa ukilinganisha na jezi za msimu wa 2019/ 20 na amewaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kununua jezi kwenye maduka yatakayotangazwa na Kampuni ya GSM tu na watawachukulia hatua wote watakaouza jezi feki.
Amewaeleza mashabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga kuwa mwaka huu wamesajili kikosi kizuri cha kupambana na timu yoyote, na kwamba matokeo ya juzi ya sare dhidi ya Tanzania Prisons ni mwanzo tu ambapo kuanzia Jumapili ijayo kikosi kitaanza kutoa burudani kwa mashabiki wake, hivyo wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kuishangilia timu yao.
Wakati huohuo, Yanga imezindua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu hiyo.

 

Leave A Reply