The House of Favourite Newspapers

Yanga Wamchunia Miloud Hamdi Licha ya Mafanikio Uwanjani


MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC inatajwa kuwa mabosi wa timu hiyo wamemchunia kwenye suala la kuanza mazungumzo naye kuongeza mkataba mpya msimu utakapogota mwisho.

Ikumbukwe kwamba Miloud alipewa kazi ya kukinoa kikosi cha Yanga SC muda mfupi baada ya Sead Ramovic kufikia makubaliano ya kuachana na kikosi hicho kinachoongoza ligi akitokea ndani ya Singida Black Stars.

Taarifa zinaeleza kuwa ni miezi sita alisaini kukinoa kikosi hicho chenye pointi 70 baada ya kucheza mechi 26 kikiwa kinaongoza kwa safu kali ya ushambuliaji ambapo ni mabao 68 wachezaji wat imu hiyo wametupia.

Miloud alitwaa tuzo ya kocha bora ndani ya Aprili baada ya kukiongoza kikosi cha Yanga kupata ushindi kwenye mechi zake nne ambazo walishuka uwanjani. Ilikuwa Tabora United 0-3 Yanga SC, Coastal Union 0-1 Yanga SC, Azam FC 1-2 Yanga SC na Fountain Gate 0-4 Yanga SC.

Yanga SC kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ujao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Mei 13 itakuwa dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Namungo FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 27 ilipata ushindi kwenye 8, sare 7 ikiambulia kichapo kwenye mechi 12 huku safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 23 na katika hayo 22 ilitupia ndani ya 18 na bao moja nje ya 18 pointi zake kibindoni ni 31.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.

JARIBIO la UBAKAJI! BIBI MIAKA 61 AVAMIWA – APIGWA MPINI wa JEMBE na KIJANA wa MIAKA 30 – AJERUHIWA