The House of Favourite Newspapers

Yanga wamepania kwelikweli hii mechi

 

YANGA wamesisitiza kwamba kilichotokea kwenye mechi ya mwisho ya Ligi dhidi ya Lipuli wakalala mjini Iringa hakiwezi kutokea Mwanza wiki ijayo.

 

Yanga inakwenda Mwanza kucheza na Alliance katika mechi ya robo fainali ya FA ambayo Kocha Mwinyi Zahera alishaweka wazi kwamba kwa namna yoyote ile hawaachi kitu kwenye mechi za mashindano hayo.

 

Kikosi cha Yanga kiliendelea na mazoezi yake ya kujifua jana katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo huku wachezaji wakijumuika katika mazoezi hayo.

 

Yanga ambayo ipo chini ya kocha msaidizi, Noel Mwandila inatarajia kuvaana na Alliance Machi 30 jijini Mwanza katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA.

 

Akizungumza na Spoti Xtra linaloongoza kwa mauzo kila Alhamisi na Jumapili, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa katika mazoezi ya jana morali ilikuwa juu na kila mchezaji anaelewa umuhimu wa mchezo huo utakaowapa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

 

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu dhidi ya Allince, leo (jana) tumefanya mazoezi Chuo cha Polisi, wachezaji wote walikuwepo, mwalimu anatumia muda huu katika kuhakiisha anakinoa vyema kikosi chake ili kiweza kufanya vyema katika mchezo huo kwani lengo ni kuhakikisha tunafanikiwa kusonga mbele.

 

“Kwa sasa bado hatujajua kikosi kitaondoka lini kuelekea Mwanza kwa kuwa bado hadi tarehe 30 hivyo muda ukifika tutaelekea huko na mwalimu Mwinyi Zahera atajiunga na timu mara baada ya kumaliza majukumu yake ya timu ya taifa,” alisema Hafidh. Heritier Makambo alikuwa mmoja wao.

 

Comments are closed.