Yanga Wampa Baraka Gadiel Kukipiga Simba

KATIKA kuonyesha kuwa hawana shida na aliyekuwa beki wao Gadiel Michael, uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa baraka zake kwa mchezaji huyo kwa kusema kuwa hawana tatizo kwa mchezaji huyo kutua Simba.

 

Gadiel Michael ambaye aliichezea Yanga misimu miwili iliyopita, ameachana na klabu hiyo kufuatia kusaini mkataba wa miaka miwili Simba hali ambayo ilizua sintofahamu kwa mashabiki wa Yanga.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa kwa upande wao hawana shida na mchezaji huyo kuondoka Yanga na kudai kuwa faili lake ndani ya Yanga lilishafungwa muda mrefu.

“Kuhusu suala la Gadiel kuondoka Yanga kwetu haina shida yoyote kwani suala lake tulishalifunga muda mrefu na hata mwenyekiti aliweka wazi, hivyo kwenda kwake Simba hakuna tatizo kwa upande wetu, tunachokiangalia ni kukiimarisha kikosi chetu.

 

“Tunaamini wachezaji tuliowasajili watafanya vyema msimu ujao katika ligi, kwani lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi kilicho imara na chenye upinzani zaidi msimu ujao,” alisema Mwakalebela./

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

NOMA! MIKAKATI Ya YANGA Hii Ni BALAA, Dismas Ten Aelezea..!


Loading...

Toa comment