The House of Favourite Newspapers

YANGA WASAINI DILINONO NA KAMPUNI YA MACRON KUTOKA ITALY

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa (katikati) akiongea na wanahabari.
Mwakilishi wa Macron, Suleman Karim (kulia) na Charles Mkwasa (katikati) wakisani mkataba.
Wakipongezana.

KLABU ya Yanga leo imeingia mkataba na Kampuni ya Macron ambao wataidhamini klabu hiyo juu ya jezi.

Mkataba huo walioingia Yanga na kampuni hiyo utakuwa wa miaka mitatu huku ukiwa na thamani ya bilioni mbili.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema: “mkataba huu unamaanisha kwamba ndiyo itakuwa dawa ya wauza jezi feki ambao walikuwa wanatupiga kabla ya kusaini mkataba huu.

“Mkataba hu utakuwa wa miaka mitatu na utakuwa na thamani ya bilioni mbili, lakini utakuwa ukiongezeka thamani kwa kila mwaka,”alisema Mkwasa.

Naye mwakilishi wa Macron, Suleman Karim alisema: “Yanga ni klabu kubwa, na tulikuwa na projeketi nao kabla ya kusaini mkataba huu.

Picha na Musa Mateja | Global Publishers

GLOBAL HABARI: MBUNGE SUGU ANYIMWA DHAMANA, ARUDISHWA RUMANDE

 

Comments are closed.