Yanga Watinga Fainali ya CRDB Federation Cup Baada ya Kuwachapa JKT Tanzania 2-0
MABINGWA watetezi wa CRDB Federation Cup, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wamekata tiketi ya kutinga hatua ya fainali.
Katika mchezo wa nusu fainali CRDB Federation Cup iliyochezwa Mei 18 2025 ubao umesoma 2-0 JKT Tanzania Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mabao ya Prince Dube dakika ya 41 kwa makosa ya safu ya ulinzi ya JKT Tanzania akiwa ndani ya 18 na bao la pili limefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 90 kwa pasi ya Clatous Chama.
Yanga SC inatangulia fainali inamsubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali kati ya Simba SC dhidi ya Singida Black.
Wababe hawa wawili Simba SC na Singida Black Stars wanatarajiwa kucheza Mei 31 2025, Tanzanite Kwaraa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.