The House of Favourite Newspapers

Yanga Wavujishiwa Siri za Ibenge Al Hilal, Wapewa Mbinu ya Kuwamaliza Mapema

0
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga.

KUELEKEA katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Msaidizi wa AS Vita, Roul Shungu, amewapa siri Yanga ambao ni mabosi wake wa zamani kwa kuwaambia wana kila sababu ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Al Hilal ya Sudan kwa kuwa wachezaji wengi wa timu hiyo wanazijua vyema mbinu za Florent Ibenge.

 

Yanga wanatarajia kucheza mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa dhidi Al Hilal, Oktoba 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, kabla ya marudiano Oktoba 15, nchini  Sudan ambao utaamua timu itakayokwenda hatua ya makundi.

Wachezaji wa timu ya Yanga wakifanya yao.

Shungu ametoa kauli hiyo kutokana na Yanga kuwa na wachezaji sita wa zamani wa AS Vita ambao wamefanya kazi na Ibenge kabla ya kutawanyika huku wachezaji hao wakiwa ni Fiston Mayele, Joyce Lomalisa, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko, Shaban Djuma na Yannick Bangala.

 

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Shungu alisema kuwa anaona nafasi kubwa kwa Yanga kuweza kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na wachezaji wengi wa timu hiyo kuzijua vyema mbinu nyingi za Ibenge ambaye alikuwa kocha wao wa zamani.

Kocha wa Al Hilal, Florent Ibenge.

“Nadhani Yanga wana nafasi kubwa sana ya kuweza kupata ushindi na kwenda hatua inayofuata kwa sababu ya mwalimu wao ameweza kuwa nao kwa muda mrefu lakini wachezaji karibu wote wamekuwa pamoja kwa kipindi kirefu tofauti na Ibenge pale Al Hilal ambayo amejiunga nayo hivi karibuni.

 

“Lakini hata wachezaji wengi waliopo Yanga ambao wametoka hapa AS Vita wanatambua vyema mbinu za Ibenge kwa sababu wamefanya naye kazi kwa muda mrefu, angalia mchezaji kama Mayele, Bangala hata Djuma ambao wote wanaingia kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga, ndiyo maana nakwambia nafasi kubwa ya kushinda ipo upande wao,” alisema Shungu.

SOPHIA AMELOWA wa HARMONIZE ANAFUNGUKA, NYUMA ya PAZIA VIDEO ya AMELOWA | MAPITO..

Leave A Reply