The House of Favourite Newspapers

Yanga Wazua Hofu Kambi ya USM Alger Kuelekea Mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho

0

HOFU ndani ya kambi ya wapinzani wa Yanga, USM Alger, imetanda kuelekea mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya wachezaji wa timu hiyo wote kupokonywa simu.Mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Jumapili hii saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, kisha marudiano Juni 3, mwaka huu huko nchini Algeria.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka moja wa mtandao wa michezo wa Algeria, zinasema kwamba uongozi wa timu hiyo, umewazuia wachezaji wake kujihusisha na masuala ya mitandao kwa kuwapokonya simu zao na badala yake kuelekeza akili zao katika mchezo wa kwanza wa fainali utakaopigwa Uwanja wa Mkapa.

Uongozi huo pia umewazuia wachezaji wake kufanya mahojiano na vyombo ya habari nchini huko ili kuzuia taarifa zao za kimbinu kujulikana na wapinzani wao, Yanga.

Licha ya taarifa zao kufichwa, lakini zipo baadhi zimevuja katika ambapo wamekuwa wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na usiku.

Program hizo mbili zinakwenda sambamba na uchambuzi wa baadhi ya video za mechi za Yanga ambazo wamezicheza hatua ya makundi, robo fainali na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Uchambuzi wa video hizo ulianza kufanyika tangu Jumapili iliyopita mara baada ya kupata chakula cha jioni wakati timu hiyo ikiwa kambini.

Ndani ya kambi hiyo, hakuna mawasiliano kutoka kwa watu walio nje ya kambi hadi hapo timu itakaposafiri kuja Dar es Salaam, Tanzania.

KAMANDA wa ZIMAMOTO ALIVYOFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MOTO UMETEKETEZA BIDHAA KIWANDANI…

Leave A Reply