The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaanika Ratiba Wiki ya Mwananchi -Video

0

Kuelekea kilele cha WIKI YA MWANANCHI Agosti 29, 2021, klabu ya Yanga imesema Wiki ya Mwananchi itazinduliwa rasmi Jumapili Agosti 22, 2021 visiwani Zanzibar lakini kilele cha Wiki ya Mwananchi itafanyika uwanja wa Mkapa, Dar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Suma Mwaitenda amesema Wiki ya Mwananchi inaashiria mambo ya fuatayo.

1. Kumalizika kwa msimu uliopita [2020/21] na kuanza kwa msimu mpya [2021/22]

2. Kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi kuelekea msimu mpya.

3. Kutambulisha wachezaji wa timu ya vijana na timu ya wanawake

4. Kuzindua jezi kwa ajili ya msimu mpya [2021/22].

Kwenye WIKI YA WANANCHI kutakuwa na shughuli za kurejesha kwa jamii kwa kutoa huduma ikiwa ni pamoja na kuchangia damu, kufanya usafi na kutoa misaada kwa wasiojiweza.

Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi atakuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla.

 

Leave A Reply