The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaachana na Lamine Moro

0

UONGOZI wa Klabu ya Yanga leo Julai 29, umethibitisha, kuachana na beki wake kisiki na nahodha Lamine Moro ambaye amedumu kwa kipindi cha miaka miwili.

 

Beki huyo na Uongozi wa Yanga wamekubaliana kusitisha mkataba, aidha uongozi umemshukuru Lamine kwa utumishi wake ndani ya Yanga.

Kwa hali hiyo Lamine hatokuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa wa kihistoria msimu ujao wa Ligi na michuano ya Kimataifa ambapo Yanga itawakilisha taifa kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

 

Leave A Reply