The House of Favourite Newspapers

Yanga Yachimbwa Mkwara Mzito

Yanga wakiendelea na mazoezi.

KUFUATIA uongozi wa Yanga kudaiwa kufanya mazungumzo na kiungo wa JKU na Zanzibar Heroes, Feisal Salum ‘Fei Toto,’ uongozi wa timu hiyo umeibuka na kusema kuwa mchezaji huyo hawezi kwenda popote. Fei Toto alianza kuonyesha kiwango kikubwa kwenye michuano ya Chalenji iliyofanyika Kenya mwishoni mwa mwaka jana na kuisaidia Zanzibar Heroes, kabla kukiwasha tena kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi akiwa na JKU.

 

Licha ya kiungo huyo kufanya siri mzungumzo yake na Yanga, lakini Championi linafahamu kuwa timu hiyo ipo kwenye mazungumzo na mchezaji huyo na muda wowote wakikamilisha huenda wakampa mkataba wa awali kabla ya kumsajili moja kwa moja katika kipindi kijacho cha usajili.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa JKU, Sadu Ally, alisema kuwa hawapingi mchezaji huyo kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine lakini hawapo tayari kuona wakifanyiwa hujuma zozote kutokana na kuwa na mkataba naye. “Tetesi nilikuwa nazisikia mpaka sasa hatujapata barua yoyote kutoka kwa kiongozi wa Simba wala Yanga zaidi ya kusikia kelele, na huyo mchezaji mwenyewe ana mkataba wa miaka mitano na ndiyo kwanza ametumikia miaka miwili na nusu bado miwili na nusu.

 

“Kumekuwa na watu wengi ambao wanamdanganya mchezaji wetu kitu ambacho siyo sahihi. Hao wanaosema wamemchukua sawa mimi nataka waje watueleze na huyo mchezaji ni nani amemruhusu kwenda huko. “Ninavyofahamu mchezaji kutakiwa na timu nyingine siyo kitu kigeni iwapo utaratibu utafuatwa na siyo kufanya ujanja, mbona walipomtaka Emmanuel Martin tuliweza kuwapatia, kwa nini huyo Fei Toto tuwazuie?” alihoji Ally.

Stori na Ibrahim  Mussa

Comments are closed.