YANGA YACHOMOA DAKIKA ZA MAJERUHI TAIFA

Bao la mkwaju wa penati la dakika ya 86 lililofungwa na Patrick Sibomana limeiwezesha Yanga kutoka sare dhidi ya Township Rollers katika michuano ya klabu bingwa Afrika hatua ya awali mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa.

 

Mchezo huo ulikuwa wa kati huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku Rollers wakionekana kucheza kwa kujiamini kana kwamba wapo nyumbani.

 

Township walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya saba lililofungwa na Phenyo Serameng baada ya kumpiga chenga mlinzi Muharami Issa ‘Marcelo’ ndani ya box na kupiga shuti la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango Metacha Mnata.

 

Yanga ilipaswa kwenda mapumziko wakiwa wamesawazisha bao hilo kwani Patrick Sibomana alikosa mkwaju wa penati dakika ya 30 baada ya Mapinduzi Balama kumshikikisha mlinzi wa Rollers.

 

Yanga itapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Botswana, Agosti 23 au kupata sare ya kuanzia mabao mawili na kuendelea.


Loading...

Toa comment