The House of Favourite Newspapers

Yanga Yafunguka Sababu ya Kumtimua Kaze

0

MWENYEKITI wa Kamati ya Ufundi ndani ya Klabu ya Yanga, Dominick Albinus amesema kuwa sababu kubwa iliyowafanya waachane na benchi lao la ufundi ni matokeo mabaya ambayo yalikuwa yakipatikana ndani ya uwanja.

 

 

Jana, Machi 7, benchi la ufundi la Yanga lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze, msaidizi wake Nizar Halfan, kocha wa viungo Edem Mortoisi, kocha wa makipa Vladimir Niyonkuru pamoja na Ofisa Usalama Mussa Mahundi walichimbishwa.

 

 

 

Mchezo wao wa mwisho ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga. Bao la Yanga lilifungwa mapema na Fiston Abdulazack likawekwa sawa na Pius Buswita dakika ya 89.

 

 

 

Mwenyekiti amesema:”Ilikuwa ni makubaliano kwetu na kila mmoja alikuwa anajua kwamba tunahitaji kupata matokeo na mwisho wa siku tumekuwa tukipata matokeo mabovu ambayo hayapendezi.

 

 

 

“Ikiwa timu haipati matokeo wa kuwatazama ni benchi la ufundi kwa kuwa wao wanatambua kwamba namna gani inahitajika kufanyika ndani ya uwanja hivyo hii ni hatua ya mwanzo na kazi inaendelea kwa wachezaji kwa kuwa nao tumewaambia kwamba wao ni sababu.

 

 

 

“Wachezaji tumewaambia kwamba tumeondoa benchi la ufundi kwa kuwa hakuna matokeo na ikitokea na wao pia tukagundua kwamba hakuna ambaye anajituma basi itakuwa kazi kwake,” amesema.

 

 

 

Kaze alisaini dili jipya ndani ya Yanga Oktoba 16 baada ya kutua usiku wa Oktoba 15 huku Nizar na Edem wakitua ndani ya Yanga Januari 27 na kufutwa kazi Machi 7.

Leave A Reply