The House of Favourite Newspapers

Yanga Yafungukia Ishu ya Kuachana na Sarpong

0

UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa bado haujaachana na mshambuliaji wao, Michael Sarpong ambaye kwa sasa ameelekea nchini China kwa ajili ya majaribio.Sarpong raia wa Ghana, ali-ibukia ndani ya kikosi cha Yanga msimu huu akitokea nchini Rwanda ambapo alikuwa anacheza Rayon Sports.

 

Ndani ya Yanga inayo-nolewa na Kocha Cedric Kaze, ametupia mabao manne kati ya 29 katika mechi 18 za Ligi Kuu Bara.Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa kuachana na mchezaji kwa wakati huu sio jambo jepesi, hivyo watu wasi-fi kirie kwamba nyota huyo ameachwa.

 

“Unafi kiri kuachana na mchezaji ndani ya Yanga ni kitu chepesi? Hilo halipo, kuna utaratibu ambao upo na kwa sasa mchezaji huyo bado ni mali ya Yanga. Ameenda China kwa majaribio tu,” alisema Mwakalebela

Leave A Reply