Kartra

Yanga Yaichapa Prisons, Yatinga Robo Fainali

GOLI pekee la mshambuliaji  Yacouba Songne dakika ya 54’ dhidi ya Tanzania Prisons limeipeleka Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho la Azam ASFC mchezo uliochezwa leo Aprili 30 kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

 

Licha ya Yanga kuihitaji ushindi huo na kutinga robo fainali lakini pia ushindi huo utaongeza morali ya timu hiyo kabla ya kuvaana watani wa Jadi Simba Mei 8, kwenye dimba la  Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kesho Mei mosi, Simba itashuka dimbani kucheza na Kagera Sugar kwenye hatua ya 16 bora ya kombe hilo, huku wakisaka nafsi ya kutinga robo Fainali.

 


Toa comment