The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaifuata Mbeya City Full Mziki

0

MSAFARA wa watu 38 ukiwa na wachezaji 24 wa Yanga na viongozi 14 wa timu hiyo, leo Alhamisi  Feb 11, 2021 wamesafiri kuwafuata Mbeya City kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa wikiendi hii.

 

Katika msafara huo, kiungo mshambuliaji raia wa Burundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ameachwa jijini Dar akipewa program maalum kutokana na kutokuwa fiti ambapo hivi sasa anafanya mazoezi ya gym.Timu hizo zinatarajiwa kuvaana keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, alisema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika na kikubwa wanakwenda Mbeya kufuata pointi tatu lengo likiwa ni kuendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi.

Mfikirwa alisema timu hiyo inatarajiwa kusafiri leo alfajiri kwa ndege ambapo wameamua kutumia usafiri huo ili kutowachosha wachezaji kutokana na umbali wa safari hiyo.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na msafara wetu utakuwa wa watu 38, kati ya yao wachezaji 24 na viongozi 14 watakaosafiri na timu,” alisema Mfikirwa huku akiwataja wachezaji watakaosafiri ni;Metacha Mnata, Farouk Shikalo, Mukoko Tonombe, Lamine Moro, Tuisila Kisinda, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Deus Kaseke na Farid Mussa.

 

Wengine ni Said Makapu, Adeyum Saleh, Paul Godfrey ‘Boxer’, Omari Chibada, Dickson Job, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne, Fiston Abdoul Razack, Haruna Niyonzima, Michael Sarpong, Feisal Salum na Carlos Carlinhos.

Leave A Reply