Yanga Yaifunga AFC Leopards Bao 1-0 Arusha, Tshishimbi Atua

KIKOSI cha Yanga leo kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa leo uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Bao la Yanga limepachikwa dakika ya 83 na nahodha wa kikosi hicho, Papy Tshishimbi akimalizia pasi ya Patrick Sibomana ambaye alipiga kona kwa guu lake la kushoto likazamishwa nyavuni na kichwa cha Tshishimbi.


Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa ulishuhudia kadi nyekundu kwa mchezaji wa AFC Leopards, Vincent Obvu baada ya kuonyeshwa kandi mbili za njano kwenye mchezo wa leo.

Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga nyanda za juu kusini baada ya mchezo wa kwanza kucheza na Polisi Tanzania na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

STORI NA LUNYAMADIZO MLYUKA, DAR


Loading...

Toa comment