The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaitwanga Majimaji 4G

KLABU ya Yanga imeinyuka kipigo kikali cha bao 4-1 timu ya Majimaji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Yanga walianza kupata bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalty kupitia kwa Papii Kabamba Tshishimbi dakika ya 20 baada ya Mpoki Mwakinyuke wa Majimaji kuunawa mpira uliokuwa ukizama kimyani.

Chirwa akapachika bao la pili kunako dakika ya 30 huku Martin akipachika bao la tatu dakika ya 44.

Marcel 56 wa Majimaji aliandika bao la kufutia machozi huku Tshishimbi akirudi na kupachika bao la nne kunako dakika ya 84.

Yanga wanabaki nafasi ya pili wakiwa na pointi 37 nyuma ya Simba wenye pointi 41.

 

Comments are closed.