YANGA YAJIPA MATUMAINI KUSONGA MBELE KIMATAIFA

MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa nafasi bado ipo kwa timu hiyo kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabinwa Afrika licha ya kulazimisha sare nyumbani.


Yanga leo, Agosti 10, 2019 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Township Rollers ya Botswana, mchezo uliochezwa uwanja Taifa.


Rollers walianza kupachika bao la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa mshambuliaji wao Phenyo Seremeg kabla ya Patrick Sibomana kuweka usawa kwa mkwaju wa penalti dakika ya 87.


Zahera amesema:’Ilikuwa ni makosa yetu kushindwa kupata ushindi mapema kwani wachezaji niliwaambia kazi ya kwanza ni kushinda nyumbani kabla ya kuwafuata huko kwao.


“Kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa kitu cha muhimu ukiwa nyumbani ni kupata ushindi kabla ya kwenda kurudiana ila bado tuna nafasi kwa kuwa nasi tumefunga bao,” amesema.


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.


Loading...

Toa comment