Kartra

Yanga Yajipigia KMKM Bao 2-0 Azam Complex

KIKOSI cha Yanga Septemba 30, 2020 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya KMKM kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

 

Mabao ya Yanga yalifungwa na Tonombe Mukoko dakika 10 kwa kona ya Carols Carinhos kiungo ambaye amepewa jukumu la kupiga mipira iliyokufa ndani ya Yanga.

 

Dakika 20 mbele Mukoko tena alipachika bao la pili na la mwisho wa timu yake baada ya mabeki wa KMKM ya Zanzibar kujichanganya katika harakati za kuokoa hatari.

Kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa KMKM kuweza kuweka mzani sawa huku Yanga nao pia wakikwama kuongeza bao la pili.

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa kirafiki ambapo lengo kubwa ni kukiweka kikosi sawa cha Yanga fiti kwa kuwa hakikuwa na mazoezi ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2020/21 kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua ratiba nyingi duniani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa malengo makubwa ni kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi zao zinazofuata.

“Kikosi kilikuwa na muda mfupi kwa ajili ya maandalizi ya ligi hivyo kwa sasa tunazidi kujiimarisha ili kuwa bora hasa ukizingatia kwamba tuna wachezaji wengi wapya,” amesema.


Toa comment