Yanga Yajipigia Mlandege FC

Timu ya Wananchi ‘Yanga’ imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandege FC ya Visiwani Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliopigwa usiku wa jana Jumanne, Novemba 9, 2021 katika Dimba la Amani Visiwani humo.

 

Yanga walikuwa wageni waalikwa katika mchezo huo ambao ni sehemu ya hafla za kutimiza mwaka mmoja madarakani kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi tangu aapishwe kuiongoza Zanzibar.

 

Bao pekee la Yanga limefungwa na Heritier Makambo raia wa Congo DR dakika ya 49 na kutosha kabisa kupeleka furaha kwa Wananchi huku likipeleka simanzi kwa Mlandege ambao walijidhatiti vilivyo kuibana Yanga tangu kipindi cha kwanza.

 

Mechi hii imepigwa ikiwa vilabu vyote vikiwa kwenye mapumziko ya kupisha timu za taifa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 kule Qatar, hii imekuwa nafasi nzuri ya Yanga wanaoongoza Ligi Kuu Bara kuendelea kujifua na hasa kuwapa mafasi wachezaji wengine ambao hawajapata mafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwenye ligi.

 

Ijumaa hii Yanga wataingia dimbani tena kumenyana na timu ya KMKM huklo huko visiani Zanzibar katika mechi nyingine ya kirafiki.2178
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment