The House of Favourite Newspapers

Yanga yakomaa na nyota sita tu

0

Yanga-training.jpgWachezaji wa timu ya Yanga wakifanya mazoezi.

Na Khadija Mngwai
TOFAUTI na timu nyingine za Ligi Kuu Bara zilizotoa wachezaji katika timu za taifa, Yanga haijalala na imeanza na mazoezi licha ya kubakiwa na wachezaji wachache kikosini.
Juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm alikuwa makini kuwafundisha wachezaji sita tu kwani wengine hawakufika mazoezini hapo huku wengi wao wakiwa timu za taifa.
Wakati Yanga inayoshika nafasi ya pili katika ligi, ikianza harakati zake za kujiandaa na mechi za ligi kuu zitakazochezwa mwezi ujao, Simba ya nne, yenyewe imepumzisha wachezaji wake hadi Novemba 17 watakapoanza mazoezi na vinara Azam FC yenyewe itaanza mazoezi Desemba 6 au 7, mwaka huu.

Walioudhuria mazoezi ya Yanga, juzi ni Thaban Kamusoko, Geoffrey Mwashiuya, Pato Ngonyani, Benedict Tinoko, Oscar Joshua na Deogratius Munishi ‘Dida’ na jana akaongezeka Deus Kaseke.

Hata hivyo, katika mazoezi hayo Pluijm aliwekea msisitizo zoezi la kupiga mashuti na namna ya kukabana ambapo kutokana na uchache wa wachezaji waliongezwa chipukizi wa kikosi cha vijana.

Wachezaji wa Yanga waliopo Taifa Stars ni Ali Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva na Malimi Busungu.

Waliopo timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes inayojiandaa na Kombe la Chalenji ni Juma Makapu na Simon Matheo. Rwanda ameenda Amissi Tambwe wakati Togo ilimchukua Vincent Bossou.

Leave A Reply