The House of Favourite Newspapers

Yanga Yakubali kichapo Cha mabao 1-3 kutoka Kwa Tabora United

0

Klabu ya soka ya Yanga imekubali kichapo Cha mabao 1-3 kutoka Kwa Tabora United, katika muendelezo wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara pale Chamazi Complex.

Magoli mawili ya Offen Chikola na bao Moja la Nelson Muganda, yalitosha kuwafanya mabingwa hao watetezi kukubali kichapo Cha pili mfululizo, baada ya kukubali kichapo Cha kwanza msimu huu dhidi ya Azam FC mwishoni mwa wiki iliyopita.

Yanga iliwakosa baadhi ya nyota wake kama Ibrahim Bacca, mwenye kadi nyekundu, Dickson Job pamoja na walinzi wa pembeni Chadrack Boka na Yao koussi wenye majeraha.

Yanga itasalia nafasi ya pili ikiwa na alama 24 baada ya michezo kumi, huku wafuga nyuki Tabora United wakiendelea kusalia katika nafasi ya sita pia wakifikisha alama 17.

Leave A Reply