KLABU ya Yanga imelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wake mkoani Morogoro waliowafanyia fujo baadhi ya mashabiki wa Simba SC waliojitokeza katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar na hivyo kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa tukio hilo.



