The House of Favourite Newspapers

Yanga yaliteka Jiji la Mbeya

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga tayari wametinga ndani ya Jiji la Mbeya kuwakabili Wajelajela Tanzania Prisons, leo Jumatatu.

Yanga ambayo ilitumia usafiri wa ndege kutua jijini hapa, imekuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yao ya hivi karibuni.

 

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga am­baye pia ndiye aliyeongo­za mapokezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe, Kayanda Sanga amewataka mashabiki na wa­nachama wa timu hiyo kuji­tokeza kwa wingi kuipasapoti timu yao.

 

“Tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kuipokea timu salama na kilichobaki ni kupambana kuhakikisha timu inapata ushindi dhidi ya Pris­ons,” alisema.

Kabla ya kukutana leo kwenye Uwanja wa Sokoine, ikumbukwe kuwa katika mch­ezo wa mwisho ambao ul­izikutanisha timu hizo katika ligi msimu uliyopita, Yanga ilikubali kipigo cha mabao mawili.

 

Kocha wa Prisons, Moham­med Abdallah, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wa­napata matokeo.

“Tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri dhidi ya Yanga kwenye mch­ezo huu, hivyo mashabiki wa­jitokeze kwa wingi,” alisema Abdallah.

DERICK LWASYE, Mbeya

Comments are closed.