The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamfuata Mrithi Wa Mayele Fabrice Ngoma Kutoka Al Hilal

0
Mshambuliaji raia wa DR Congo, Makabi Lilepo.

MARA baada ya Yanga kufikia hatua nzuri ya kumsajili kiungo Fabrice Ngoma kutoka Al Hilal, imebainika kwamba klabu hiyo imeanza mpango wa kufanya usajili wa mshambuliaji raia wa DR Congo, Makabi Lilepo akitajwa kwamba ndiye atakuwa mrithi sahihi wa Fiston Mayele.

Yanga tayari wameweka wazi mipango yao ya kuhakikisha msimu ujao wanafanya vema katika michuano ya kimataifa ambapo watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimu huu wa 2022/23, Yanga ilianzia Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ilipoteleza, ikaangukia Kombe la Shirikisho Afrika na kufika hadi fainali.

Chanzo cha ndani kutoka DR Congo, kimelipa taarifa Yanga juu mpango wao wa kukamilisha usajili wa wachezaji hao wote wawili kutoka Al Hilal, licha ya Simba nao kumuhitaji Makabi Lilepo.

“Yanga baada ya kufikia pazuri kwenye usajili wa Fabrice Ngoma, sasa wamehamishia nguvu zao kuhakikisha wanamsajili Makabi Lilepo ambaye wanaamini wakimpata utakuwa usajili mzuri kwao kutokana na uchezaji wake kuendana na Yanga.

“Yanga wanafahamu kuwa Simba wapo kwenye mazungumzo na Lilepo, lakini wanachokifanya ni kuamini katika mpango wao, hivyo kwa sasa ninavyokwambia Yanga mpango wao ni kuwapata wachezaji hao wote wawili raia wa DR Congo.

“Wote ni wachezaji ambao wanapatikana kwa sasa kutokana na hali ilivyo nchini Sudan, huku michezo ikiwa haiendelei, hivyo uongozi wa Al Hilal upo kusikiliza ofa za wachezaji, ni suala la viongozi wa timu husika kupeleka ofa,” kilisema chanzo hicho.

STORI NA MARCO MZUMBE

FEI TOTO AZUNGUMZA AKIWA AZAM – ”TAFANYA KAMA YANGA, TUTACHUKUA UBINGWA”…

Leave A Reply