The House of Favourite Newspapers

Yanga Yanga Princess ‘Ubingwa Lazima’

0

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga Princess, Edna Lema amefunguka kuwa, mpaka sasa bado hakuna uhakika wa bingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake, licha ya tofauti ya pointi moja Simba Queens.

 

Yanga Princess walipoteza uongozi wa ligi baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita.

 

Simba inaongoza msimamo ikiwa na pointi 39, huku Yanga Princess wao wakiwa katika nafasi ya pili na pointi zao 38 baada ya wote kucheza mechi 15 Akizungumza na Championi Jumamosi, Edna alisema:

 

“Bado kikosi changu kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri msimu huu, na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake licha ya kwamba tuko nyuma kwa pointi na viongozi wa msimamo Simba Queens.

 

“Pointi moja kwenye soka ni ndogo sana, na lolote linaweza kutokea hivyo kila mtu acheze na kushinda mechi zake, kuhusu bingwa tutamjua mwishoni.”

Leave A Reply