The House of Favourite Newspapers

Yanga yapewa Ndanda, Simba Coastal Kombe la FA

0

Omari Mdose,

Dar es Salaam

DROO ya mechi za robo fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Kombe la FA ilitolewa jana ambapo Yanga itacheza na Ndanda FC huku Simba ikipangwa kucheza na Coastal Union ya Tanga.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), katika robo fainali ya Kombe la FA, Machi 31, 2016, Yanga itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo pia, Azam FC itacheza na Prisons kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Simba imepangwa kucheza na Coastal Union, Aprili 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Machi 26, mwaka huu, Geita Gold itacheza na Mwadui FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Baada ya mechi hizo, Aprili 7, itachezeshwa droo ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo itaonyeshwa ‘live’ runingani. Bingwa wa kombe hilo atapata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Leave A Reply