The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapiga Hesabu Kali Kombe la FA

0

UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa kama siyo mchezo wao wa Kombe la FA kusogezwa mbele basi wangekuwa mkoani Katavi kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mchezo huo.

Yanga ilitarajiwa kuvaana na Tanzania Prisons katika mchezo huo Aprili 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Rukwa jirani na Katavi.

 

Mchezo huo umesogezwa mbele kupisha maombolezo ya siku 21 ambazo wamezitangaza Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kufuatia kifo cha hayati, John Pombe Magufuli.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema lengo la kwenda kuweka kambi Katavi ni kwa ajili ya wachezaji wao kuzoea hali ya hewa ya baridi iliyopo Rukwa.

 

Bumbuli alisema kuwa walifanya hivyo baada ya kupokea mapendekezo ya Bechi la Ufundi la timu hiyo lililo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.Aliongeza kuwa, ratiba ya kwenda Katavi wameisimamisha kwa sasa hadi watakapopokea ratiba mpya kutoka TFF kuhusu mchezo huo.

 

“Moja ya malengo yetu tuliyoyaweka msimu huu ni kuchukua Kombe la FA pamoja na ligi kuu.“Tunashukuru kwenye ligi tumeanza vizuri kwa kukaa kileleni katika msimamo, hivyo basi malengo yetu ni kuendelea kukaa kileleni hadi mwishoni mwa msimu tuwe mabingwa.

 

“Hivyo ni lazima tufanye maandalizi ya mapema ili kufanikisha kupata matokeo mazuri dhidi ya Prisons, tunafahamu siyo mchezo mwepesi kwetu kutokana na ubora wa wapinzani, lakini tutapambana kupata matokeo mazuri,” alisema Bumbuli.


Leave A Reply