The House of Favourite Newspapers

Kisa Derby, Yanga Yapigwa Faini ya Milioni 3

0

Klabu ya Yanga leo Julai 8, 2021 imetozwa faini ya Shilingi Milioni 3 kwa kufanya makosa kwenye mechi dhidi ya Simba SC Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kutumia mageti ya uwanja wa Uhuru kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu.

° Kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu.

° Kuingia uwanjani kupasha misuli kwa kutumia mlango ambao haukupangwa kutumika kwa namna yoyote.

° Kutumia chumba cha wafanya usafi wa uwanja kubadilisha nguo badala ya chumba maalum cha kubadilishia nguo.

Na pia klabu ya Yanga inatakiwa kulipa Shilingi laki nane na nusu (850,000) ikiwa gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wakiingia uwanjani pamoja na makufuli ya uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoharibiwa katika tukio hilo.

Leave A Reply