The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapokea Kipigo Cha Kwanza Ligi Kuu Bara

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC leo wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United ‘Chama la Wana’, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Bao pekee kwenye mchezo huo, lilifungwa na Pastory Athanas, dakika ya 58 akiachia shuti kali mbele ya mabeki, Haji Mwinyi na Vincent Bossou.

Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Mlandizi, wenyeji Ruvu Shooting walitoshana nguvu na Toto Africans kwa matokeo ya suluhu.

yanga-line-latestKikosi kamili cha timu ya Yanga.

Na Leonard Msigwa/GPL

 

Comments are closed.