The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapunguza Hasira Kwa Ndanda

0

BAADA ya Yanga kucheza kwa dakika 270 bila ya kuambulia pointi tatu ndani ya Ligi Kuu Bara, hatimaye jana ikapunguza hasira zake mbele ya Ndanda FC.

 

Kabla ya mchezo huo wa jana uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar, Yanga ilicheza mechi tatu ambazo ni sawa na dakika 270 na kuambulia sare zote. Matokeo ya mechi hizo ni; JKT Tanzania 1-1 Yanga, Yanga 0-0 Azam na Yanga 2-2 Namungo.

 

Katika mchezo wa jana ambao Yanga walikuwa wanakamilisha ratiba kutokana na Simba kuwa mabingwa, Wanajangwani hao walitangulia kufunga bao kupitia Deus Kaseke dakika ya sita.Ndanda walipofungwa bao hilo, wakaja juu na kusawazisha kupitia kwa Abdul Hamis dakika ya 10 na Omary Mponda (dk 16). Dakika ya 45+1, Kaseke akasawazisha na kuwa 2-2.

Kipindi cha pili Yanga ikaongeza bao la tatu kupitia kwa Mrisho Ngassa dakika ya 74 ambapo kiungo huyo mshambuliaji aliingia dakika ya 64 kuchukua nafasi ya Ditram Nchimbi.Jana ilishuhudiwa David Molinga ambaye aliibuka shujaa katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo kwa kufunga mabao mawili, alianza kikosi cha kwanza cha Yanga kisha kutolewa dakika ya 77 kumpisha Patrick Sibomana.

 

Ushindi wa jana umeifanya Yanga kufikisha pointi 60 katika nafasi ya pili na kuwa nyuma ya vinara Simba kwa pointi 18 huku ikibakiwa na mechi sita. Ikishinda zote itakuwa na pointi 78 ilizonazo Simba hivi sasa ambayo ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

STORI: JOEL THOMAS,DAR ES SALAAM

Leave A Reply