The House of Favourite Newspapers

Yanga Yashtukia Hujuma Ligi kuu Bara

0

BAADA ya kukusanya pointi tisa kwenye michezo mitatu ya Ligi kuu Bara msimu huu, Yanga wameanza kushtukia mipango inayotajwa kufanyika na wapinzani wao ili kuivurugia katika malengo yao ya kubeba ubingwa msimu huu.

 

Kikosi cha Yanga kwa sasa kinajiandaa na mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Azam FC utakaopigwa Oktoba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Taarifa ilizozipata Spoti
Xtra kutoka chanzo cha ndani cha Yanga, zinaeleza kuwa: “Kuna watu wanafanya hujuma ili Yanga waweze kufeli kwenye mzunguko wa kwanza na kutoka kwenye malengo ya ubingwa kama ilivyokuwa msimu uliopita.

 

“Viongozi hivi karibuni walikaa na wachezaji ambao hawapati namba kwenye kikosi kwa ajili ya kushirikiana kuhakikisha ubingwa unarejea nyumbani msimu huu.


“Wanaotuhujumu
tumeshagundua na kwa sasa wanataka kuanza kwenye mechi inayofuata dhidi ya Azam.”
Makamu Mwenyekiti wa
Yanga, Fredrick Mwakalebela, aliliambia Spoti Xtra kuwa:


“Ni kweli tumesikia hizo
hujuma zinazofanywa kwa ajili ya kututoa kwenye mbio za ubingwa msimu huu, hivyo niwatoe wasiwasi Wanayanga kuwa mapungufu yote tuliyokuwa nayo msimu uliopita ya kutuhujumu hayawezi kujitokeza msimu huu.


“Suala la kambi
tumeshalifanyia kazi na tutaendelea kuwa Avic Town kama kutakuwa na mabadiliko tutawaambia,
mpaka sasa tumeshadhibiti
kila kitu, kuhusu usalama tumeweka wa kutosha.”

Leave A Reply