The House of Favourite Newspapers

Yanga Yashusha Kiungo wa Kimataifa

0

YANGA imepania kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi ni baada ya kumshusha kiungo mshambuliaji matata, Godfred Nyarko anayekipiga klabu ya Medeama ya nchini Ghana.

 

Yanga imebakisha nafasi mbili za wachezaji wa kimataifa ambayo tayari ina kumi pekee ambao ni kipa Djigui Diarra, Klahid Aucho, Jesus Moloko Mukoko Tonombe, Yacuoba Songne, Yannick Litombo, Said Ntibanzonkiza ‘Saido”, Shaban Djuma na Heritier Makambo.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, kiungo yupo nchini zaidi ya wiki moja akiendelea kuangaliwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi huko kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Mtoa taarifa huyo alisema upo uwezekano mkubwa wa kiungo huyo mwenye kasi, uwezo mkubwa wa kupiga pasi, kuchezesha timu na kufunga mabao akapewa mkataba wa awali kabla hajasajiliwa rasmi dirisha dogo.

 

Aliongeza kuwa kiungo huyo atasajiliwa katika dirisha dogo msimu huu baada ya benchi la ufundi na uongozi kukubali uwezo wake katika mazoezi ya timu hiyo.

 

“Nyarko yupo kambini kwa zaidi ya wiki moja akiendelea kufanya mazoezi pamoja na timu huku akisubiria usajili wa dirisha dogo litakapofunguliwa.

 

“Kama unakumbuka tulibakisha nafasi mbili za usajili kati ya 12 tulizoruhusiwa kusajili katika usajili huu mkubwa ambao tayari umefungwa.

 

“Na Nyarko ni kati ya wachezaji tuliopanga kuwasajali kuchukua nafasi moja kati ya hizo mbili tulizobakisha ambaye hivi sasa yupo kambini anaendelea mazoezi pamoja na wenzake,”alisema mtoa taarifa huyo.

WILBERT MOLANDI NA IBRAHIM MUSSA, Dar

Leave A Reply