The House of Favourite Newspapers

Yanga Yataja Warithi wa Lamine, Sarpong

0

KAMA mpango wa Yanga wa kuachana na wachezaji wake, Lamine Moro na Michael Sarpong ukatimia, basi huenda mshambuliaji wa AS Vita, Fiston Mayele na beki wa DC Motema Pembe, Henock Inonga wakachukua mikoba yao.

 

Lamine na Sarpong, inaelezwa kwamba mwishoni mwa msimu huu watapewa mkono wa kwaheri ndani ya kikosi hicho huku sababu kubwa ikiwa ni utovu wa nidhamu.

 

Chanzo chetu cha uhakika kutoka Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, kamati ya nidhamu ya timu hiyo, itakaa hivi karibuni kwa ajili ya kujadili ishu zote za utovu wa nidhamu zilizotokea ndani ya kikosi hicho kisha majibu watayapeleka kamati tendaji na kuweka hadharani hatma za wachezaji hao.

Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, mbali na hilo, hivi sasa Yanga ipo katika mazungumzo ya kuwasajili wachezaji wawili, mshambuliaji na beki mmoja wa kati ambao ni Henock Inonga na Fiston Mayele.

 

Kmati ya Nidhamu ya Yanga hivi karibuni itakaa kujadili mambo mengi yaliyojiri ya kinidhamu, hivyo suala la Lamine Moro na Michael Sarpong yatajadiliwa, kisha kurudishwa kamati tendaji na hapo ndiyo itafahamika kama wachezaji hao watabaki Yanga au wataondoka.

 

“Lakini hayo yakiendelea, Yanga pia ipo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao ni mshambuliaji wa kati na beki mmoja wa kati kwa ajili ya kukiimarisha kikosi kuelekea msimu ujao.

 

Wachezaji hao ni Henock Inonga anayecheza nafasi ya beki wa kati na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji wa kati, hayo ni moja kati ya majina yaliyomo katika orodha ya wachezaji walio katika mazungumzo na uongozi wa Yanga,” Kilisema chanzo hicho.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominick Albinus, aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Kila kitu kuhusu maamuzi ya wachezaji wenye matatizo ya kinidhamu yanafanyiwa kazi na Kamati ya Nidhamu ya Yanga.“Watu wanatakiwa kusubiri kwani kabla ligi haijamalizika Kamati ya Nidhamu itakuwa imeshakamilisha mambo yao na kila kitu kitafahamika.”

MARCO MZUMBE,Dar es Salaam

Leave A Reply