The House of Favourite Newspapers

Yanga Yateka Shoo

0

SIMBA na Yanga zimemwaga mkwanja mrefu msimu huu ili kuhakikisha zinashindana haswa kuwania mataji mbalimbali ambayo timu hizo zinashiriki msimu huu.

 

Tangu Yanga ianze kupewa sapoti na Kampuni ya GSM dirisha dogo la msimu 2018/19 imekuwa ikishusha majembe kila msimu ili kushindana na Simba ambayo hadi wakati huo ilikuwa inatawala ligi kiasi cha kubeba mataji manne mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Kama kawa dirisha kubwa la mwaka huu pia timu hizo vigogo kutoka ndani ya Mkoa wa Dar zilishikana vilivyo sokoni ili kuhakikisha zinavuta wachezaji ambao wanaona watazisaidia kufanya kweli msimu huu.

 

Matajiri kutoka GSM na kule Simba kuna mwekezaji Mohammed Dewji ambaye tangu arudishe majeshi yake hapo Simba imekuwa ikifanya vizuri ndani ya uwanja.

 

Championi Jumatano, limefanya utafiti kwa viongozi wa timu hizi za Simba na Yanga ili kupata thamani ya kila mchezaji ambaye yupo ndani ya vikosi hivyo.

 

Baada ya hapo, wababe wa soka hapa wakakupangia kikosi kulingana na ukubwa wa thamani ya mchezaji kutokana na nafasi anayocheza ndani ya uwanja.

 

Kipa; Djigui Diarra huyu ni kipa wa Yanga ambaye ametua kikosini hapo dirisha kubwa kwa dau la Sh mil 350 akitokea Stade Malien ya nchini kwao Mali, hapa ‘sub’ wake atakuwa Manula ambaye anakipiga Simba na thamani yake ni Sh mil 100.

 

Beki ya kulia atasimama Djuma Shaban wa Yanga ambaye ametua kikosini hapo kwa Sh 500m na mpinzani wake ni Shomari Kapombe wa Simba ambaye thamani yake ni Sh mil 80.

 

Ubavu wa kushoto moja kwa moja Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ anaingia kikosi cha kwanza kutokana na dau lake la Sh mil 100 alilopewa juzikati wakati akisaini Simba. Mpinzani wake ni David Bryson wa Yanga aliyevuta Mil 30.

 

Pale beki ya kati kuna vita kubwa sana lakini mastaa Bakari Mwamnyeto wa Yanga ameingia kikosi cha kwanza akisajiliwa kwa Sh mil 200 na yeye atacheza na Pascal Wawa wa Simba ambaye alitua kikosini hapo kwa Sh Mil 100.

 

Hao jamaa wakichoka watasaidiwa na Joash Onyango aliyevuta Mil 80, huku Dickson Job wa Yanga akisajiliwa kwa dau la Mil 50.

 

Nafasi ya kiungo mkabaji Mganda wa Yanga, Khalid Aucho moja kwa moja ana uhakika wa kuanza kutokana na kutua kikosini hapo kwa dau la Sh mil 450 akimzidi Thadeo Lwanga wa Simba aliyetua kwa Mil 80 akiwa mchezaji huru.

 

Eneo hili pia kuna Mukoko Tonombe wa Yanga aliyechukua Sh 290Mil wakati Sadio Kanoute wa Simba akichota Sh 350Mil na Jonas Mkude Sh 100Mil.

Nyuma yao kuna Zawadi Mauya alisajiliwa kwa dau la Mil 30, wakati Mzamiru Yassin wa Simba akichukua Mil 50.

 

Viungo washambuliaji, anakaa Larry Bwalya akiwa amechukua Sh 200Mil huku akiwa na Peter Banda, Duncan Nyoni na Ousmane Sakho ambao kila mmoja alichukua Sh 350Mil hawa wote wanakipiga Simba.

 

Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyesajiliwa kwa dau Sh 100Mil na dau lake limeongezeka baada ya Simba kuingia kwenye vita na Yanga. Yacouba Songne raia wa Burkina Fasso amechukua Sh 90Mil, Farid Mussa 100Mil, Deus Kaseke 50 sawa na Ditram Nchimbi.

 

Kwa upande wa mawinga, Jesus Moloko wa Yanga alichukua Sh 220Mil akizidiwa na Bernard Morrison aliyepewa Sh 136Mil na Simba.

 

Kwa upande wa washambuliaji, Yanga yupo Heritier Makambo aliyevuta Sh 380Mil, Fiston Mayele amechukua mil 250 na kinda Yusuph Athumani akiweka kibindoni Sh 50Mil.

 

Simba wenyewe yupo Meddie Kagere aliyechukua Sh 150Mil, Chriss Mugalu 120Mil na John Bocco 100Mil baada ya kusaini mkataba mpya katika msimu huu.

Musa Mateja na Wilbert Molandi

Leave A Reply