The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Kibabe -Video

0

HISTORIA Imeandikwa baada ya klabu ya Yanga kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza ikiwa ugenini katika Uwanja wa Royal Bafokeng, mjini, Rustenburg nchini Afrika Kusini.

Yanga imetinga fainali hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushinda mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants kwa mabao 2-0, na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1, kwani katika mchezo wa kwanza ikishinda 2-0, nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kazi kubwa imefanywa na wachezaji wote wa Yanga wakiongozwa na Nasreddine Nabi ambaye ni Kocha Mkuu.

Ni Fiston Mayele alianza kupachika bao la kuongoza kwa Yanga dakika ya 44 kisha ngoma ikapachikwa na Kenned Musonda dakika ya 67.

Musonda alimalizia kazi ya Mayele na kufanya Yanga kuwa mbele kwa jumla ya mabao 4-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa Yanga ilishinda mabao 2-1.

Bao pekee la Marumo iliyokuwa nyumbani limefungwa na Chivaviro dakika ya 90 lakini ni la kufutia machozi tu.

Yanga wanatinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni kazi kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Historia imeandikwa, hongereni Yanga.

Leave A Reply