The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatoa Dozi Pemba

0
Wachezaji wa timu ya Yanga wakiongea jambo

 

KIKOSI cha Yanga kilichojikita kisiwani Pemba, jana Alhamisi kilijitupa dimbani kumenyana na wenyeji wao, Kombaini ya Chakechake ambapo kwenye mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Gombani, kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuonyesha uwezo mzuri.

Yanga chini ya kocha wake, George Lwandamina, imejichimbia kisiwani hapa ikijiweka sawa kabla ya kuwavaa Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Agosti 23, mwaka huu.
Katika mchezo huo ambao licha ya Yanga kutumia vikosi viwili, iliibuka na ushindi huo mwembamba kwa bao lililofungwa na mshambuliaji wake mpya, Ibrahim Ajibu katika dakika ya 25.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Licha ya washambuliaji wa timu hiyo kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini kuzitumia vema hali iliyomfanya Lwandamina baada ya mchezo kukaa vyumbani na Matheo Anthony na Amissi Tambwe na kuanza kuwapa darasa la kuwa makini wawapo langoni baada ya kukosa nafasi nyingi za mabao.
Kikosi cha Yanga kilichoanza kilikuwa hivi;

Rostand Youthe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Raphael Daud, Thaban Kamusoko, Said Makapu, Emmanuel Martin, Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu.
Kikosi kilichocheza kipindi cha pili ni Ramadhan Kabwili, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Maka Edward, Juma Mahadhi, Baruan Yahya, Yussuf Mhilu, Said Mussa na Amissi Tambwe.

Stori: Abdi Suleiman | Championi Ijumaa

Leave A Reply