Kartra

Yanga Yatoa Jipya Kuhusu Metacha

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu hatma ya kipa wao namba moja Metacha Mnata kwa kuwa bado ni mali yao kwa sasa.

 

Mnata kwa sasa yupo ndani ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ilikuwa kambi nchini Kenya na inatarajia kesho kumenyana na Equatorial Guinea kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON.

 

Ndani ya Yanga, msimu wa 2020/21 Mnata amekusanya jumla ya clean sheet 11 alikuwa anatajwa kuondoka ndani ya timu hiyo huku watani zao wa jadi Simba wakitajwa kuitaka saini yao.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa hakuna tatizo lolote kati yao Yanga na Mnata wanachojua wao ni mchezaji halali wa timu hiyo.“Hakuna tatizo lolote kati ya Yanga na Mnata, yeye ni mchezaji wetu na kwa sasa yupo kambini na timu ya taifa ya Tanzania hivyo mashabiki wasiwe na mashaka,” alisema.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam


Toa comment