The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatoa Tamko Mchezo Dhidi Ya Simba Uko Pale Pale

Hali ya mpambano kati ya Simba SC na Yanga SC imechukua sura mpya ya sintofahamu. Simba SC wamesema hawatacheza mechi baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi yao ya lazima uwanjani, wakidai haki zao zimekiukwa. Kwa upande mwingine, Yanga SC wamesisitiza kuwa mechi itaendelea kama ilivyopangwa leo usiku na hakuna mabadiliko yoyote.

Kwa sasa, mashabiki wanabaki na maswali mengi: Je, Simba watashikilia msimamo wao na kutosimama uwanjani? Je, Yanga watajitokeza peke yao? TFF na waandaaji wa ligi watachukua hatua gani?