Yanga Yatua Gor Mahia Kumalizana na Straika Kiboko

HESABU za mabosi wa Yanga kwa sasa ni kuhakikisha wanamalizana na straika, Dickson Ambundo ambaye alikuwa anaichezea Gor Mahia ya Kenya.

 

Mabosi hao wameafikiana kwa pamoja kuwa wamalizane fasta na Ambundo ambaye amemalizana na Gor Mahia baada ya msimu huu kumalizika ambapo klabu hiyo imemruhusu kutua sehemu yoyote kutokana na mkataba wake kuisha.

 

Yanga wanamuangalia straika huyo kama mbadala wa David Molinga ambaye inatajwa kumalizana na RS Bercane ya Morocco. Habari ambazo Spoti Xtra limezipata ni kuwa, Yanga wapo mstari wa mbele kumalizana na staa huyo wa zamani wa Alliance ya Mwanza.

 

“Kwa sasa hesabu ni kuona Ambundo anakuwa miongoni mwa wachezaji ambao watavaa uzi wa Yanga kwa msimu ujao ambapo mipango hiyo inaendelea taratibu.“Imekuwa rahisi kumpata kwa sababu tayari ameshamalizana na Gor Mahia ambapo alikuwa akicheza baada ya mkataba wake kumalizika, hivyo kwa sasa yupo huru.

 

“Tunachotaka kuona ni kwamba kabla ya wiki mbili zile za mapumziko kumalizika basi kila kitu kiwe kimekamilika na aungane na wenzake mapema kwa ajili ya kambi kwa sababu yupo hapa nchini,” kilisema chanzo.

 

Hivi karibuni, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wameshamaliza usajili wao kwa asilimi 90 kwa kufuata ripoti waliyoachiwa na aliyekuwa kocha wao, Mbelgiji Luc Eymael.

 

Yanga SC kumalizana na straika wa KenyaYanga yapeleka mkataba wa Morrison FIFA, Darkusema limeisha lakini watu wanaamua kulikuza wakati mambo yapo wazi.

 

“Hata Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanalijua jambo hilo, mashabiki wasiwe na presha, viongozi tupo na tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa,” alisema Mwakalebela.

LUNYAMADZO MLYUKA, Darr SAID ALLY

Toa comment