The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamwacha Carlinhos Dar Wakitua Mtwara

0

WAKATI kikosi cha Yanga kikitarajia kuondoka leo kuelekea Mtwara kumenyana na Namungo, timu hiyo itawakosa wachezaji wawili ambao ni Carlos Carlinhos na Balama Mapinduzi.

 

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kinatarajia kumenyana na Namungo katika mchezo wa ligi Mei 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi ukiwa ni mzunguko wa pili.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro alisema kuwa: “Timu itaondoka kesho (leo) kuelekea Mtwara kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Namungo.

 

“Kuna asilimia kubwa tukaondoka na ndege ila bado nafanya mawasiliano na kocha pamoja na Kampuni ya Precision Air ili kupata utaratibu mzuri.“Kuelekea huko wachezaji wawili watakosekana katika msafara huo akiwemo Carlos Carlinhos na Balama Mapinduzi.

 

“Kiwanja cha Majaliwa ni kigumu hivyo tunaenda mapema ili wachezaji waweze kuzoea mazingira“Chochote kitatokea na Namungo ni miongoni mwa timu ambazo zinatusumbua hivyo kupitia kocha mpya tunaamini tunaenda kupata pointi tatu,” alisema Kandoro

Leave A Reply