Kartra

Yanga Yavunja Kambi Morocco, Wakutana na Simba Airport

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesitisha ratiba ya kambi yao ya nchini Morocco na kutangaza rasmi kurejea jijini Dar es Salaam kumalizia maandalizi yao kwa ajili ya msimu ujao.

 

Uamuzi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Eng. Hersi Said na kusema kuna sababu mbalimbali zilizowapelekea klabu hiyo kufanya maamuzi hayo magumu.

 

Aidha, Eng. Hersi amesema kumeguka kwa baadhi ya wachezaji wao ambao wanatakiwa kujiunga na timu za taifa ndio sababu ya kwanza ambapo jumla ya wachezaji wao nane kuitwa katika timu zao za taifa.

 

Kwa upande mwingine, baadhi ya wachezaji wa Simba na Yanga wamekutana katika Uwanja wa ndege nchini Morocco kwa ajili ya safari ya kurejea Dar es Salaam. Hata hivyo, Klabu ya Simba bado haijatoa taarifa yoyote kuhusu iwapo wamevunjwa kambi yao ama wameruhusu baadhi ya wachezaji kwenda kujiunga na timu zao za taifa.


Toa comment