The House of Favourite Newspapers

Yanga Yawabadilishia Mbinu Waarabu

0


Wilbert Molandi, Dar es Salaam, Championi Ijumaa
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema ili wapate ushindi wa ugenini, basi lazima
wawafunge wapinzani MC Alger ndani ya dakika 15 za mwanzoni kwa lengo la kuwapa presha.
Yanga wanatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Stade 5 July 1962 uliopo kwenye Mji wa Ben Aknoun, Algeria unaoingiza mashabiki 64,000 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.Mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa ni Mzambia, Obrey Chirwa.

Wilbert Molandi (kushoto) akiongea na wachezaji wa Yanga.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwambusi alisema; “Ninaamini bao la mapema la dakika 15 za mwanzoni ni njia pekee ya kuwaondoa MC Alger, kwani timu ngeni inapopata ushindi wa mapema inawaondoa mchezoni wenyeji kwa kucheza kwa presha.
“Ninaamini uwezekano upo kwani tunao washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao ambao ni (Donald) Ngoma na (Amissi) Tambwe waliopona majeraha yao.

Leave A Reply