The House of Favourite Newspapers
gunners X

Yanga yawafuata rasmi Zanaco

KLABU ya Yanga SC, leo jioni imekwea pipa kuelekea nchini Zambia, kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.

Yanga na Zanaco zitacheza mchezo wa marudiano kwenye Uwanja Nkoloma, Lusaka, Zambia, keshokutwa Jumamosi.

Yanga imeondoka na msafara wa watu 20, ikiwa ni Benchi la Ufundi , wachezaji na viongozi. Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na timu hiyo katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Mussa Mateja/GPL

Comments are closed.