The House of Favourite Newspapers

Yanga Yawapeleka Mwakalebela, Msolla TFF

JUMLA ya wagombea 26 wa Yanga wanafanyiwa usaili utakaofanyika leo Jumapili katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 5. Miongoni mwao yupo Kocha Msomi, Mshindo
Msolla na Fredrick Mwakalebela kigogo wa zamani wa TFF.

 

Yanga inafanya uchaguzi wake Mei tano mwaka huu. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Malangwe Nchungaela amesema kuwa wagombea watakaoingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi watajulikana baada ya mchakato wa leo.

 

“Nawaomba wanachama wote wawe watulivu katika kipindi hiki wakati tunafanya mchakato wa uchaguzi ili kila kitu kiweze kwenda sawa, wanachama watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale watakaokuwa na kadi tu hivyo tunawaomba waende kulipia kadi zao,” alisema Nchungaela.

Wagombea ambao wamechukua fomu katika nafasi ya Mwenyekiti ni Msolla, Lucas Mashauri na Elias Mwanjala huku katika upande wa makamu wapo, Fredrick Mwakalebela, Thobias Lingalangala na Samweli Lukumay.

 

Katika nafasi ya wajumbe wapo, Ally Sultan, Saad Khimiji, Hassan Hussein, Siza Lyimo, Hamad Islam,
Shafiru Makosa, Injinia Leonard Marango, Cyprian Musiba na Injinia Bahati Mwaseba Wengine ni pamoja na Seif Hassan, Haruna Batenga, Nassor Matuzya, Abdallah Chikawe, Hussein Nyika, Rodger Gumbo, Said Ntimizi, Palina Conrad, Elius Mkumbo na Suma Mwita ambao wataungana na wale wa awali.

Comments are closed.