The House of Favourite Newspapers

ads

Yanga Yawatimua Kazi Makocha wa Timu ya Yanga Princess

0

KLABU ya Yanga imetangaza kuachana na makocha wawili wa timu ya wanawake ya klabu hiyo ya Yanga Princess, makocha hao ni Edna Lema maarufu kama Mourinho pamoja na Kocha msaidizi Mohamed Hussein (Mmachinga).

 

Katika taarifa iliyotolewa na mitandao ya kijamii ya klabu hiyo haijabainisha sababu hasa za kutimuliwa kwao.

Yanga Princess iliambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate FC

Klabu ya Yanga imewashukuru makocha hao na kuwatakia heri katika hatua nyingine ya Maisha yao nje ya klabu hiyo kongwe.

 

Aidha taarifa kutoka klabu ya Yanga imebainisha kuwa Klabu itatoa taarifa kuhusiana na mbadala wa nafasi hizo hivi karibuni.

 

Yanga Princess imeanza vibaya mashindano ya Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya timu ya wanawake ya Fountaine Gate FC.

Leave A Reply